MAPOKEZI YA WANAFUNZI

Chuo Cha SAUT ARUSHA kipo katikati ya Jiji la Arusha na Taarifa za msingi ni kama ifuatavyo:

1. USAFIRI – Chuo kipo Jirani kabisa ya stand kuu ya mabasi Arusha, pia kinapakana na stand ya daladala zote za Arusha Mjini (Walking distances). Hivyo ni rahisi kufika chuoni nyakati zote bila usumbufu wowote.

Usafiri wa kutoka stand kuu ya mabasi kuja chuoni ni kwa kutumia bodaboda, bajaji au tax. Hata hivyo umbali wa stand na chuoni ni mdogo Sana, na Wanafunzi hupokelewa chuoni muda wowote hata nyakati za usiku.

2.CHAKULA – Chuo Cha SAUT ARUSHA kipo karibu kabisa na soko kuu la wakulima la Kilombero ambalo ndilo soko linalopokea chakula chote kutoka kwa wakulima. Bei za vyakula ni nafuu Sana sawa na bure.

Soko Hilo pia ndilo linalouza Vifaa vingine kama mavazi, vyombo, Vifaa vya kusoma n.k kwa bei nafuu Sana.

MAPOKEZI NA KUWASILI CHUONI

Chuo kitaanza kuwapokea wanafunzi wapya kuanzia tarehe 16/10/2023 na Masomo yataanza tarehe 24/10/2023. Wanafunzi wanaotoka nje ya Arusha watapokelewa na kupewa hifadhi ya Siku 3 mpaka 5 za mwanzoni Katika hostel za chuoni bure, huku wakifanya maamuzi wa mahali pa kwenda Kuishi.

Karibuni Sana